
📘 Book Title | Tabaqat Warathat Al Anbiyai Juzuu Al Awwal |
👤 Book Author | AL MUSTAKSHIF ABU MANAL DANAH |
🖨️ Total Pages | 713 |
👁️ Book Views | 237 total views, 1 views today |
🌐 Language | English |
📥 Book Download | PDF Direct Download Link |
🛒 Get Hardcover | Click for Hard Copy from Amazon |
Tabaqat Warathat Al Anbiyai – JUZUU Al AWWAL. – Matabaka Ya Warithi Wa Mitume – Juzuu ya kwanza. Kimetayarishwa Na Kukusanywa Na Al Mustakshif Abu Manal Danah.
TABAQAT WARATHAT AL ANBIYAI – JUZUU AL AWWAL
Kuhusu Kitabu:
Kitabu chenye kuzungumzia kuhusiana na historia za miongoni mwa Wanazuoni waliotangulia kabla yetu, kulingana na Darja zao na jitihada zao na matunda ya jitihada zao hizo ambazo zinaendelea kuunufaisha Umma wa Kiislam kwa Ujumla, na hivyo namuomba Allah Subhanah wa Ta’ala awalipe Wanazuoni kwa jitihada zao kwa malipo ya kuwaingiza kwenye rehma zake na kuwajaalia Pepo zenye darja ya juu Miongoni mwa Pepo zake.
Kwani ni kutokana na Jitihada zao Wanazuoni hawa ndio sisi Waislam wa leo tumefikiwa na neema ya manufaiko ya Ilm zao hapa tulipo katika wakati wa Uhai wetu..Alhamd Lillah. Namuomba Allah Subhanah wa Ta’ala pia atuwezeshe kua ni miongoni mwa watakaokua ni wenye kunufaika na Ilm zao na kua ni wenye kufuata nyayo zao, kwani kutokana na kufuata hatua za Nyayo zao Wanazuoni hao basi ndio kwenye kupatikana Uongofu, kwani wao ni miongoni mwa walioongozwa na Allah Subhanah wa Ta’ala na hivyo sisi hatuna budi isipokua kufuata Nyayo zao na hii ni kutokana na kama tulivyoona kulingana na hadith kua Wanazuoni ni Warithi wa Mitume.
Na kutokana na kua Wanazuoni ndio Warithi wa Mitume basi pia inatubidi tujue historia za Maisha yao, ili tupate kujua namna walivyokua wakiishi katika nyakati zao, na jitihada zao kwa ajili ya Uislam, kwa ajili ya Akhera yao na kwa ajili ya Mola wao, ili angalau nasi tupate kuona mifano hai ya kuiiga kutokana na mafunzo ya kusoma historia za Maisha yao kulingana na Tabaqat za Nyakati za Maisha yao.
To read more about the Tabaqat Warathat Al Anbiyai Juzuu Al Awwal book Click the download button below to get it for free