Book Title | Wenye Azma Thabit Zaidi Miongoni Mwa Mitume 2 |
Book Author | AL MUSTAKSHIF ABU MANAL DANAH |
Total Pages | 999 |
Book Views |
|
Language | English |
Book Download | PDF Direct Download Link |
Get Hardcover | Click for Hard Similar Copy from Amazon |
WENYE AZMA THABIT ZAIDI MIONGONI MWA MITUME – SEHEMU YA PILI
ULU AL A’AZMI MINA ALRRUSUL
AL MUSTAKSHIF ABU MANAL DANAH
أولوا العزم من الرسل
WENYE AZMA THABIT ZAIDI MIONGONI MWA MITUME
Sura ya kwanza
Bila ya shaka katika aya za Qur’an nilizoanza nazo ndani ya kitabu hiki na nyenginezo
nyingi zilizomo ndani ya Qura’an tumeona kua Allah Subhanah wa Taála ametuwekea
wazi kua ndani ya kitabu chake mna muongozo wa kina wa kila kitu katika maisha yetu,
ikiwemo pia Muongozo dhidi ya matatizo mbali mbali ya kidunia na kiakhera, lakini hata
hivyo kamwe hatutoweza kuikimbia hali ya matatizo tuliyokua nayo wakati bado tukiwa
ni wenye kuutupa ufunguo unaofungua mlango wa utatuzi wa matatizo hayo,
ufunguo ambao si mwengine bali ni Qurán yenyewe ambayo ndani yake hamna Muongozo tu,
lakini pia mna Kinga, Rehma na Tiba pia ya maradhi tofauti kuanzia ya Kimwili,Kinyoyo, Kinafsi, Kiroho n.k kama inavyoweka wazi aya ifuatayo:
ونترل من القرآن ما هو شفاء ورمة المؤمنين ولا يزيد الظليين إلا
خسارا
Wanunazzilu mina alqur-ani ma huwa shifaon warahmatun lilmu/mineena wala yazeedu aldhdhalimeena illa khasaran (Surat Al Isra 17:82)
Tafsir: Na tumeiteremsha hii Qur’an ndani yake mkiwa na Tiba na Rehma kwa Walioamini, lakini kwa Madhalimu haiwanufaishi na chochote isipokua Hasara.
camini, lakini kwa Mare Anasema Sultan al Mutakallimin Muja Naam aya imetumia neno Shifaun ambalo ni lenye kutokana na neno Shafa.
Na kwa kilugha basi neno Shafa hua ni lenye kumaanisha Kuponya, Kutibu, Kurudisha Afya,
Kuridhisha, Kurudisha katika hali yake ya Asili au ya Kimaumbile, na ndio maana wenye Lugha yao hua wanasema:
Shaf’ahu aAn Al Mas-alati kumaanisha kua Amemuondolea Mashaka na kumridhisha Nafsi yake juu ya Jambo fulani.
Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Umar Ibn Al Husayn Al Taymi Al Bakri Al Tabaristan Fakhr Ad Din Al Razi Al Shafii kuhusiana na ayah hii kua: Quran ni Tiba ya Kitabia, Kijamii, Kiroho na
Kiafya pia.
Na bila ya shaka baadhi ya Aya zake zimebainika kua ni Tibba ya Maradhi tofauti ya Kimwili’
Ama kwa upande mmoja basi Hujjat Ul Islami Mujaddid Ad Din Imam Abu Hamid Ibn
Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al Shafii anatuambia
kua miongoni mwa manufaa yanayohitajika kupatikana katika Quran basi ni kujua darja
za usomaji wake katika hali tofauti kwa kusema kua: ‘Amesema Amir ul Muuminina
Ali Ibn Abi Talib kua:
‘Yeyote yule atakaesoma Qur’an wakati akiwa amesimama kwenye Sala basi anapata thawabu 100 kwa kila herufi moja ya Qur’an, na
atakaesoma Qur’an wakati akiwa amekaa kitako ndani ya Sala basi hua ni mwenye
To read more about the Wenye Azma Thabit Zaidi Miongoni Mwa Mitume 2 book Click the download button below to get it for free
Report broken link
Support this Website
Click here to join our Telegram group for new Books