
| Fataawa Arkanul Islam |
| Jopo La Wanafunzi, Uthaymin, Yunus Kanuni Ngenda |
| 927 |
| |
| PDF Direct Download Link |
| Click for Hard Copy from Amazon |
FATAAWA ARKANUL ISLAM – Sampuli
FATAAWA ARKANUL ISLAM
Swali la 1: Ni nini Tauhidi, na ni vipi vigawanyo vyake?
Jibu: Neno Tauhidi katika lugha ya kiarabu, ni kukifanya kitu kuwa kimoja na hilo haliwezi kukamilika isipokuwa kwa kukataa baadhi ya vitu na kuthibitisha baadhi ya vitu, kwa mfano tunas- ema: haitokamilika Tauhidi ya mtu mpaka kwanza ashuhudie ya kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu Mmoja tu, atakapo kuwa amesema maneno haya atakuwa amekataa ya kuwa hakuna Uungu kwa yeyote isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu peke yake.
Na kukataa huku hakumaanishi kuwa hakuna vinavyo abudiwa visivyo kuwa Mwenyezi Mungu hapana, vipo viabudiwa vingine lakini kuabudiwa kwake sio sahihi.
Ni kama unapo sema: Mtu Fulani amesimama maneno haya hayamaanishi kuwa hakuna mwingine aliye simama bali inaweze- kana kuna watu wengine wamesimama pia, lakini unapo sema: Hakusimama yeyote, ina maana hakuna mtu yoyote aliye si- mama, hapa umekataa kusimama kwa yeyote yule na unapo sema: Hakusimama isipokuwa Zaidi hapa unamaanisha hakuna yeyote aliye simama isipokuwa huyu mmoja tu ambaye ni Zaidi, na hii ndiyo Tauhidi, haiwi isipokuwa kwa kukataa vitu na kuthibitisha vitu.
Na Tauhidi katika sheria ya Kiislamu ni: kumpekesha Mwe-nyezi Mungu katika yale mambo yanayo muhusu.
Vigawanyo vya Tauhidi.
Wanachuoni wamesema Tauhidi imegawanyika ka-tika sehemu tatu nazo ni:
1-Tauhidi Rububiyyah (kumpwekesha Mwenyezi Mungu ka-tika umbaji, umiliki na upangaji).
2-Tauhidi Uluhiyyah (kumpwekesha Mwenyezi Mungu katka ibada). 3-Tauhidi Asmaa wa Swifaat (kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika majina na sifa zake).
2-Wanachuoni wamevipata hivi vigawanyo kwa kuangalia Aya na Hadithi za Mtume rehma na amani ziwe juu yake! Zilizo zungumzia mas’ala ya Tauhidi ndio wakapata ya kuwa imegawa-nyika katika sehemu hizo tatu, na tutaeleza kila kigawanyo kwa urefu zaidi.
1-Aina ya kwanza ni: Tauhidi Rububuyyah, nayo ni kump-wekesha Mwenyezi Mungu katka uumbaji, umiliki na upangaji, na ufafanuzi wake ni kama ifuatanyo;
Katika kigawanyo hiki kuna vitu vitatu muhimu:
1-kuhusu kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika uumbaji wake:
Mwenyezi Mungu peke yake ndiye muumba wa kila kitu, hakuna muumbaji asiyekuwa yeye anasema Mwenyezi Mungu: [Je kuna muumba mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu ambaye anapekuni riziki kutoka katika mbingu na ardhi, hapana Mola mwingine ila Yeye ] [Suratul Nahli].
Mwenyezi Mungu peke yake ndie muumba, ameumba kila kitu kisha akakikadiria makadirio yake mpaka vitendo afanyavyo mwanadamu Mwenyezi Mungu ndie aliye viumba kwa ajili hiyo utaona katika ukamilifu wa kuamini makadirio ya Mwenyezi Mungu ni kuamini kuwa Mwenyezi Mungu ndiye aliyeumba matendo ya waja kama alivyo sema Mwenyezi Mungu :[Na hali Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni nyinyi na hivyo mna-vyo vifanya!]. [Surat Swaafaati: 96], na hilo ni kwa kuwa ma-tendo ya Mwanadamu ni katika sifa Zake na Mja ni kiumbe wa Mwenyezi Mungu na mwenye kukiumba kitu ndie muumba wa sifa zake.
Mtu anaweza kuuliza: tutatofautishaje kati ya uumbaji wa Mwenyezi Mungu na uumbaji ambao unaweza kutokea kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu, kama ilivyo katika maneno yake Mwe-nyezi Mungu: [Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji.] [Suratul Muuminuna: 14], na maneno yake Mtume rehma na amani ziwe juu yake kwa wale wenye kupiga picha: (Kutasemwa kuwaambia vitieni roho vile mlivyo viumba) [Imeipokea Bukhary /2105/na Muslim /2107/].
Jibu la swali hilo ni kama ifuatavyo:
Asiekuwa Mwenyezi Mungu haumbi kama anavyo umba Mwenyezi Mungu, kwasababa yeye hawezi kukileta kitu am-bacho hakipo na wala hawezi kumfufua aliye kufa bali uumbaji wa asiye kuwa Mwenyezi Mungu unakuwa ni kukibadilisha kitu kutoka kwenye sifa fulani kwenda kwenye sifa nyingine bali ni kile kile kiumbe cha Mwenyezi Mungu ndio amekibadilisha.
Mfano mtu akipiga picha kitu chochote hakuleta kitu kipya bali atakuwa amebadili kitu kukipeleka kwenye kitu kingine, kama vile ambavyo mtu anaweza kubadili udongo akaufanya kama ndege au akaufanya kama picha ya Ngamia.
Na hii ndio tofauti kati ya uumbaji wa Mwenyezi Mungu na uumbaji wa asiye kuwa Mwenyezi Mungu, na kwa ajili hiyo anakuwa Mwenyezi Mungu ni mpweke kwa uumbaji unaom-husu Yeye tu.
1-Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika umiliki wake. Mwenyezi Mungu peke yake ndiye mmiliki wa kila kitu kama alivyo sema: [Ametukuka yule ambae katika mikono yake kuna ufalme naye kwa kila kitu ni muweza] [Suratul Mulku] akasema tena Mwenyezi Mungu: [Sema ni nani mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu ,naye ndiye anaye linda wala hakilindwi asicho taka,kama mnajua] [Suratui Muuminun].
Mwenye Ufalme wa wafalme wote ni Mwenyezi Mungu peke yake ufalme ambao umeenea katika kila kitu na kunasibisha ufalme kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu ni kunasbisha kwa ziada tu, na Mwenyezi Mungu amethibitisha ufalme kwa asiye kuwa Yeye pale alipo sema: [Isipo kuwa kwa wake zao au wale walio wamiliki katika mikono yao] [Suratul Muuminun].
Na Aya nyingene nyingi zinazo thibitisha ufalme kwa asiye kwa Mwenyezi Mungu, lakini ufalme huu sio kama ufalme wa Mwenyezi Mungu, kwani ni ufalme ambao una mapungufu na ni ufalme ambao unamipaka hauenei katika kila kitu, kwa mfano, nyumba anayo imiliki Omar haimiliki Zaid na nyumba anayo im-iliki Zaidi haimiliki Omar.
Kisha umiliki huu una mipaka, kuwa haruhusiwi mtu kukitu-mia kile anacho kimiliki isipokuwa atumie kama alivyo amrisha Mwenyezi Mungu, utaona kwa ajili hiyo amekataza Mtume rehma na amani ziwe juu yake! kupoteza mali hovyo, na amesema Mwe-nyezi Mungu: [Wala msiwape wasio na akili mali yenu ambayo Mwenyezi Mungu ameijaalia iwe ni kiamu yenu] [Suratul An Nisaa], na hii ni Ushahidi ya kuwa umiliki wa mwanadau una ma-pungufu kisha ni wenye mipaka, na hii ni kinyume na Ufalme wa Mwenyezi Mungu kwani ufalme wake ni wenye kuenea kila kitu usio na mipaka, na Mwenyezi Mungu hufanya analotaka na wala haulizwi kwa lile analo lifanya, lakini Mwanadamu ni mwenye kuulizwa kwa kila anacho kifanya.
3-Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika upangiliaji wake.
Yeye Mwenyezi Mungu ndie anaye pangilia mambo yote ya viumbe wake na yeye ndiye anaye endesha mambo yote katika aridhi na mbinguni amesema Mwenyezi Mungu: [Fahamuni! Kuumba na amri zake Ametukuka Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe nyote] [Suratul Araaf].
Na kupangilia huku kumeenea kila kitu hakuna kizuizi wala hakuna mwenya kupinga upangaji wake.
Na kupangilia anako pangilia mwanadamu mambo yake ya kila siku kama kupangilia kuhusu mali zake aziendeshe vipi, na watoto wake awalee vipi na mengineyo, huo ni mpangilio mfinyu na wenye mipaka ni tofauti na mipangilio ya Mwenyezi Mungu ambayo ni mipana na haina mipaka.
2-Aina ya pili katika aina za Tauhidi ni Tauhiidul Uluuhi-yyah
(Kumpekesha Mwenyezi Mungu katika Ibada)
Nayo ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika Ibada, mwa-nadamu asiabudu pamoja na Mwenyezi Mungu kitu kingine na asijikurubishe kwa kitu chochote kama anavyo jikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.
Na aina hii ya Tauhidi ndio ambayo wamepotea kwayo wen-gi katika Washirikina ambao Mtume Rehma na amani ziwe juu yake! aliwapiga vita na kuhalalisha damu zao, mali zao, ardhi yao, nyumba zao na wanawake zao pamoja na watoto wao. Na ndio Tauhidi ambayo Mwenyezi Mungu aliwatuma kwayo Mitume na akashusha Vitabu pamoja na Tauhidi Rububuyya na Tauhidi Al-Asmaa wa Swifaat, lakini zaidi walicho kuwa wanakitibu Mitume kwa watu wao ni Tauhidi hii, ambayo ni Tauhiidul Uluuhiyyah, ili Mwanadamu asimfanyie Ibada yeyote asiye kuwa Mwenyezi Mungu, awe Malaika au Mtume au Walii au Mtu mwema, au ki-umbe chochote katika viumbe vya Mwenyezi Mungu, kwasababu Ibada haiswihi kwa kitu chochote isipokuwa Mwenyezi Mungu.
To read more about the Fataawa Arkanul Islam book Click the download button below to get it for free
or
Report broken link
Support this Website
for websites