Skip to content
Home » IJTIHAD NA TAQLID pdf book download for free swahili

IJTIHAD NA TAQLID pdf book download for free swahili

IJTIHAD NA TAQLID
  • Book Title:
 Ijtihad Na Taqlid
  • Book Author:
AL MUSTAKSHIF ABU MANAL DANAH
  • Total Pages
928
  • Book Views:

Loading

  • Click for the  
PDF Direct Download Link
  • Get HardCover  
Click for Hard Copy from Amazon

IJTIHAD NA TAQLID – Sampuli

IJTIHAD NA TAQLID

MAANA YA SHARIA’H NA TASHRI’I

Neno Sharia’h kilugha maana yake ni ‘Njia inayopitwa sana kuelekea kwenye chanzo cha maji’ ambacho ni chanzo cha uhai wa kila kiumbe na vile vile a njia ilinyooka. Qur’an imetumia mara kadhaa neno Sharia’h ikiwemo katika aya zifuatazo:-

(لِكُلٍّ جَعَلْنَا مِنكُمْ شِرْعَةً وَمِنْهَاجًا ۚ)

Likullin jaAAalna minkum shirAAatan waminhajan (Surat Al Maidah 5:48)

Tafsir: Kwa kila mmoja miongoni mwenu tumekujaalieni Sharia’h na njia iliyowazi. (hapa neno Shir`at limetumika kumaanisha njia,mfumo au mpangilio).

atika Qur’an pale Allah Subhanahu wa Ta’ala alipomwambia Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kua:

(شَرَعَ لَكُم مِّنَ الدِّينِ مَا وَصَّىٰ بِهِ نُوحًا وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَمَا وَصَّيْنَا بِهِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَىٰ ۖ أَنْ أَقِيمُوا الدِّينَ وَلَا تَتَفَرَّقُوا فِيهِ ۚ)

SharaAAa lakum mina alddeeni ma wassa bihi noohan waalladhee awhayna ilayka wama wassayna bihi ibraheema wamoosa waAAeesa an aqeemoo alddeena wala tatafarraqoo feehi (Surat Ash Shuraa 42:13)

Tafsir: Yeye (Allah) amekuwekea juu yenu Shara’a katika dini ile ile kama aliyomuwekea Nuh, na kama tuliyokushushia wewe (Muhammad), na tuliyomshushia Ibrahim, Musa na Isa ili kusimamisha Dini na msifanye mfarakano ndani yake.

Ingawa nimeitumia aya hii kwa ajili ya kufafanua maana ya neno Sharia’h lakini pia aya hii ni aya ya pili iliyowataja Ulul A’zmi wote kwa pamoja baada ya ya ile aya tuliyoiangalia mwanzo tulipozungumzia Ulul A’zmi katika Surat Al-Ahzab 33:7.

Hivyo kulingana na aya tulizoziangalia hapo juu tunaona kua Sharia’h maana yake hua ni mfumo au njia ya kuelekea kuliko kusudiwa na Allah Subhanahu wa Ta’ala ambae ndie muanzilishi na muumbaji wa kila kilicho hai. Vile vile tukiangalia katika mtizamo wa Fiqh basi tunaona kua Sharia’h maana yake ni njia iliyowekwa na Allah Subhanahu wa Ta’ala kwa ajili ya kufuatwa na Bani Adam.

Tashri’i maana yake ni njia ya kuisimamia Sharia’h, hivyo kufanya Tashri’i humaanisha kuweka au kufuata njia za kanuni na maelekezo ya mpangilio na mfumo ambao wahusika wanatakiwa kuufuata ipasavyo ili kuwapatia Bani Adam mafanikio ya Maisha ya Duniani na Akhera.

Mukhtasar wa mfano wa mafanikio hayo hua yanaonekana wazi pale tunapoiangalia Hadith maarufu iliyomo katika Sahih Muslim ambayo hua inayojulikana kama Hadith ya Jibril A’layhi Salaam isemayo kua:

Anasema Umar Ibn Khattab kua: ‘Siku moja wakati tukiwa tumekaa na Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, ghafla alitokea mtu mmoja ambae alikua amevaa nguo nyeupee na nywele zake zilikua nyeusii, lakini hata hivyo hakuonekana kua ni mtu ambae alikua ni mwenye kutoka safarini. Na hakuna hata mmoja miongoni mwetu ambae aliekua akimjua mtu huyo.

Mtu huyo alikuja akakaa kitako mbele ya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, kiasi ya kua magoti yake yakagusana na magoti ya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, kisha akaiweka mikono yake juu ya magoti ya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam na kusema: ‘Ewe Muhammad! Hebu nielezee kuhusiana na Uislam.’

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Uislam ni kushuhudia kua hakuna Mungu isipokua Allah na Muhammad ni Mtume wake; na Kusali, kkah, na kufunga Ramadhani, na kuenda Makkah Kuhiji kwa mwenye uwezo.’

Yule mtu akasema: ‘Umesema ukweli’, hivyo nasi tukashangaa kua yeye ndie alieuliza suali na kisha yeye yeye ndie anaethibitisha jibu lake.’

Kisha akauliza, ‘Niambie kuhusiana na Iman.’

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Ni kuamini juu ya Allah, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Mwisho, na Qadar – uzuri wake na ubaya wake.’

Yule mtu akasema: ‘Umesema ukweli, sasa niambie kuhusiana na Ihsan.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Ni kumtumikia Allah kama kwamba unamuona, na kama humuoni basi kwa hakika yeye hua anakuona.’

Yule mtu akasema: ‘Umesema ukweli, sasa niambie kuhusiana na Saa ya mwisho.’

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Yule aneulizwa hajui kitu kuhusiana na hilo kuliko yule anaeuliza.’

Yule mtu akasema: ‘Niambie kuhusiana na dalili zake.’

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Ni pale wanawake watumwa watakapozaa mabibi zao; na utakapoona wanaotembea bila ya viatu, bila ya nguo, na mwanzo wa wachunga kondoo kushindaniana kujenga majumba marefu.’

Kisha yule mtu akaondoka, nami nikasubiri kwa muda mrefu. Kisha Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akaniuliza : ‘Jee unamjua ni nani yule aliekuja kuuliza masuali. Ya Umar?’

Nami nikajibu: ‘Allah na Mtume wake wanajua zaidi’, nae Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Yule alikua ni Jibril. Alikuja kukufundisheni dini yenu.(Sahih Muslim)

Katika Hadithi hii tunaona kua, wakati alipoulizwa kuhusiana na Uislam na Iman Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam alijibu sehemu zinazoyajumuisha mambo hayo kwa pamoja, na alipoulizwa kuhusiana na Ihsan, basi tunaona kua alizungumzia kuhusiana na Tabia na Maadili. Hivyo, kulingana na msingi wa Hadith hii, Wanazuoni wa Sharia’h ya Dini ya Kiislam wameigawa I’lm ya mafunzo ya Sharia’h katika sehemu tatu ambazo ni A’qai’d, Akhlaq na Ahqam.

(i) A’qai’d (Aqida): Haya hua ni mafunzo ya mambo ambayo ni lazima yafahamike na pia yanatakiwa yaaminiwe kwa kila Muislam. Mambo haya yanajumuisha ingi ya Iman kama vile, umoja wa Allah Subhanah wa Ta’ala, Sifa zake, Mitume wake, Vitabu vyake na mambo mengineyo.

I’lm ya mafunzo haya hujulikana kama, I’lm al Aqaid. I’lm hii tutaiangalia kwa

undani zaidi mwishoni mwa sura ya tano.

(ii) Akhlaq (Maadili): Haya hua ni mafunzo ya mambo ambayo yanahusiana na maamrisho na ushughulikiaji wa Nafsi na Tabia za Bani Adam kama vile uadilifu, ucha Mungu, ushujaa, usafi, busara, ustahmilivu, ukweli, uaminifu n.k kwa kuonesha namna gani Bani Adam anatakiwa awe. I’lm ya mafunzo haya hujulikana kama, I’lm al Akhlaq.

Allah Subhanahu wa Ta’ala katika kutuonesha mfano wa Akhlaq anasema katika

Qur’an kwa kumuambia Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kua:

(إِنَّكَ لَعَلَىٰ خُلُقٍ عَظِيمٍ)

Wa-innaka laAAala khuluqin AAadhdheemin (Surat Al Qalam 68:4)

Tafsir: Na hakika, wewe (Ewe Muhammad) ni mwenye khuluq bora kabisa.

Anasema Abu ‘Ali Ahmad Ibn Muhammad Ibn Ya’qub Ibn Miskawayh katika kuielezea maana ya neno Khuluq ambayo wingi wake ni Akhlaq katika kitabu chake, kua : ‘Khuluq ni hali ya Nafsi inayoipelekea kufanya vitendo bila ya kuhitaji haja ya kutafakari au haja ya kua na kusudio. Hali hii huweza kugawika katika sehemu mbili: Kwanza ni kua hali ya maumbile na hua ni sehemu ya tabia halisi ya mtu, kama vile kucheka sana kwa kila kitu kinachomfurahisha, au kuhuzunika kutokana na kitu chochote kibaya kitakacho mtokezea.

Hali ya pili ni ile yenye asili ya kulelewa na kufundishwa kikawaida, na ingawa inaweza kua ina asili ya kutokana na kutafakkar na pia kukusudia lakini hatimae hua ni sehemu ya tabia.’(Tahdhib Al Akhlaq)

Imam Abu Hamid Ibn Muhammad Al Ghazal yeye anasema kuhusiana na Khuluq katika kitabu chake cha Ihya Ulum Din kua : ‘Khuluq ni jina la hali ya kitu chenye asili ya kina na ithabati katika Nafsi, hali ambayo husababisha vitendo kutekelezeka kwa urahisi na kwa utaalamu bila ya kuwepo na haja ya kutafakari au kukusudia. Na inapofikia kiasi ya kua hali hii inazalisha ndani ya Nafsi vitendo vizuri na vya kupendeza kutokana na mtizamo wa ufahamu na wa Sharia’h basi hio hua ni Tabia nzuri; Na inapofikia kiasi ya kua hali hii inazalis Nafsi, basi hio hua ndio Tabia mbaya.

To read more about the Ijtihad Na Taqlid book Click the download button below to get it for free

or

Report broken link
Support this Website


for websites

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *