Skip to content
Home » Kuutembelea Msikiti Ntukufu Wa Mtume pdf download

Kuutembelea Msikiti Ntukufu Wa Mtume pdf download

KUUTEMBELEA MSIKITI NTUKUFU WA MTUME
  • Book Title:
 Kuutembelea Msikiti Ntukufu Wa Mtume
  • Book Author:
Abdallah Bin Najiy Al Mikhlafy
  • Total Pages
44
  • Book Views:

Loading

  • Click for the  
PDF Direct Download Link
  • Get HardCover  
Click for Hard Copy from Amazon

KUUTEMBELEA MSIKITI NTUKUFU WA MTUME – Sampuli

KUUTEMBELEA MSIKITI NTUKUFU WA MTUME

Sehemu ambazo inafaa kwa Muislamu kuzitembelea

katika mji mtukufu wa Madina nje ya Msikiti mtukufu wa Mtume:

1- Baqii: Nayo ni sehemu ya makaburi ya watu wa Madina, na hapo wamezikwa Maswahaba wengi na Matabiina na wema wengine waliotangulia radhi za Allah na rehema zake ziwe juu yao, Mtume rehma na amani ziwe juu yake alikuwa akiwa tembelea waliozikwa Baqii na kuwasalimia na alikuwa anawaombea dua.

Utakapo enda Baqii wasalimie waliozikwa pale, na useme kama alivyokuwa akisema Mtume wetu rehma na amani ziwe juu yake:(Assalaamu alaykum ahlu ddiyaari minal muuminiina wal muslimiina, wa innaa inshaa LLahu laahiquuna, as’alu LLaha lanaa walakumul A’fiyah). maana yake: Amani iwe juu yenu watu mliozikwa (hapa) miongoni mwa waumini na waislamu, na hakika bila ya shaka tutakutana Allah akipenda, namuomba Allah atujaalie afya sisi na nyinyi.Ameipokea Imamu Muslim Allah amrehemu.Na uwaombee watu wa Baqii na uwatakie msamaha kwa Allah, hiyo ndiyo ziara ya kisheria.Na jihadhari ndugu yangu muislamu usikanyage juu ya kaburi au kulikalia, hakika imepokewa kutoka kwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake ya kwamba alikataza hilo pindi aliposema:((Msiswali makaburini, wala msiyakalie makaburi)).Ameipokea Imamu Muslim Allah amrehemu.

Na jihadhari kutokana na kupangusa makaburi au kuyabusu au kuchukua mchanga katika makaburi au kuwaomba watu wa makaburini kwani wao hawawezi kudhuru wala kunufaisha.

2- Kutembelea Mashahidi wa vita vya Uhdi: Navyo ni vita vilivyo tokea baina ya waislamu na makafiri, katika vita hiyo wakufa wakiwa mashahidi Maswahaba sabini radhi za Allah ziwe juu yao, na Mtume rehma na amani ziwe juu yake alikuwa akiwazuru mashahidi wa Uhdi akiwasalimia na kuwaombea, na elewa ya kwamba hao mashahidi waliuliwa wakati wakiilinda dini, na miongoni mwa haki zao juu yetu ni kuwaombea na kuwatakia radhi za Allah ziwe juu yao wote, kwahiyo pindi utakapo wazuru basi wasalimie kama ulivyo wasalimia watu wa Baqii na wengineo katika watu waliokufa.

3- Masjid Qubaa: Ni sheria kutembelea Masjid Qubaa na kuswali ndani yake, Mtume rehma na amani ziwe juu yake alikuwa akienda Masjid Qubaa kila wiki kwa kipando au kwa miguu na anaswali nadani yake, na mwenye kwenda Masjid Qubaa na akaswali anapata malipo ya aliyefanya Umrah, amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake:((Mwenye kujitwaharisha katika nyumba yake kisha akaenda kuswali Masjid Qubaa anapata malipo kama ya mtu aliyefanya Umrah)).Ameipokea Imamu Ibni Maajah Allah amrehemu.

Ndugu yangu muislamu usiinyime nafsi yako kheri hii kubwa.

Angalizo na muongozo kwa mwenye kuutembelea Msikiti wa Mtume rehma na amani ziwe juu yake:

Ndugu mgeni mtukufu:

Jitahidi kufanya adhkaar zilizo thibiti wakati wa kuingia na kutoka katika Msikiti wa Mtume rehma na amani ziwe juu yake, au ufanye hivo katika Misikiti mingine.

Usiiname wakati wa kumsalimia Mtume rehma na amani ziwe juu yake, lakini unatakiwa usimame kwa utulivu na adabu.

Usijipanguse kuta au nguzo zilizopo ndani ya Msikiti wa Mtume au milango au Mimbari au Mihirabuni au madirisha yaliyopo upande wa chumba cha Mtume, kujipangusa kwa ajili ya kutaka baraka, kwasababu haijuzu kufanya hivo.

Amesema Imamu Nawawiy Allah amrehemu, katika kitabu: “Al Majmuu” (8/257): Kutokana na kupangusa kwa mkono kaburi la Sharifu: “Na mwenye kufikiria ya kwamba kupangusa kaburi kwa mkono kunaleta baraka zaid, basi mtu huyo yupo katika ujinga na ameghafilika, kwasababu baraka ni ile iliyo wafiqiana na sheria, vipi utapata baraka kwa jambo ambalo liko kinyume na usawa”.

Ndugu yangu mgeni elewa ya kwamba kuzuru maeneo tajwa hakufungamani na muda maalum: Muda mchache au mwingi , wala hakufungamani na swala maalum, chache au nyingi, na miongoni mwa makosa wanayofanya wenye kuuzuru Msikiti mtukufu wa Mtume ni kwamba wanadhani kuwa ni lazima waswali ndani ya Msikiti idadi ya swala maalum, ima swala arobaini au mfano wa hayo, na baadhi ya watu wanazipa uzito nafsi zao na kuwadhiki wengine, na hilo ni kosa, kwasababu haikuthibiti kwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake kuweka idadi maalum ya swala anazo takiwa kuswali mtu mwenye kuuzuru Msikiti wake, bali swali swala unazoweza (zilizo thibiti) ziwe nyingi au chache.

Na hadithi iliyopokelewa inayo zungumzia juu ya swala arobaini katika Msikiti wa Mtume ni ile iliyokuja katika Musnadi Imamu Ahmad kutoka kwa Anas bin Maalik radhi za Allah ziwe juu yake, kutoka kwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake:((Mwenye kuswali katika Msikiti wangu swala arobaini bila kupitwa na swala hata moja, ataandikiwa na Allah kuwa yuko mbali na Moto, na ataokolewa kutokana na adhabu, na atawekwa mbali na unafiki)).Hadithi hii ni dhaifu.Na ama hadithi nyingine ambayo ameitoa Imamu Tirmidhiy kutoka kwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake amesema:((Mwenye kuswali kwa ajili ya Allah siku arobaini kwa jamaa na kwa kuipata takbira ya takbira ya kwanza, ataandikiwa kuokoka kutokana na mambo mawili: kuokoka kutokana na Moto, na kuokoka kutokana na unafiki)).Hadithi hii imethibiti kwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake.

Kwa ajili hiyo mimi ninakuusia ndugu yangu mgeni ujipatie utakaso huo sawa umeijua hadithi hii ukiwa Madina au umeijua ukiwa katika mji wako.

Asili ni kwamba mwenye kuomba anatakiwa aelekee Kibla wakati wa kuomba dua, na baadhi ya watu wanasimama pembezoni mwa Msikiti wa Mtume wananyoosha mikono yao na kumuomba Allah Mtukufu hali ya kuwa wameelekea kaburi tukufu la Mtume, jambo hilo halikupokelewa kwa wema walio tangulia wa umma huu, wala kwa Maimamu wao na Wanachuoni wao walio bora, chukua tahadhari ndugu yangu mgeni kutokana na matendo kama hayo, na yakutoshe yale yaliyo watosha Maswahaba wa Mtume rehma na amani ziwe juu yake, na waliokuja baada yao na wema walio tangulia katika waumini, hakika ya dua Kibla yake ni Al Kaabah.

Haijuzu kuandika ujumbe ambao ndani yake kuna maombi ya kumuomba Mtume rehma na amani ziwe juu yake kisha kuuweka katika madirisha ya chumba cha Mtume au kuuweka Raudhwa au upande wowote katika Msikiti wa Mtume, kwasababu huo ni uovu na ni jambo lililo katazwa, na vilevile haifai kubeba ujumbe kutoka miji tofauti na kuupeleka katika Msikiti wa Mtume.

Haijuzu (kutufu) kulizunguka kaburi la sharifu, Twawafu ni ibada ambayo haijuzu kufanywa sehemu yoyote isipokuwa katika Al Kaaba tukufu katika kumtukuza Allah Mtukufu na kutekeleza amri yake.

Fanya bidii ndugu yangu mgeni kwa kufanya sana twaa na mambo ya kheri kwa muda ambao utakuwepo katika mji mtukufu wa Madina, na jitahidi kuswali swala za faradhi kwa jamaa katika Msikiti wa Mtume na uzidishe kuswali swala za Sunna katika Raudhwa tukufu -ikiwa hilo litakuwa jepesi kwako- kwasababu imethibiti kwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake alisema:

((Sehemu iliyopo baina ya mimbari yangu na nyumba yangu ni kiwanja katika viwanja vya Peponi)).

Ameupokea Imamu Bukhary na Muslim Allah awarehemu.

Na kuihusisha sehemu hiyo kuliko sehemu nyingine katika Msikiti ni dalili kuwa ni sehemu bora kuliko nyingine, basi fanya bidii kuswali swala za Sunna katika sehemu hiyo na kumtaja Allah na kusoma Qur’an bila ya kusongamana na kuwaudhi wanaoswali, kwasababu mwenye kuacha jambo kwa ajili ya Allah, basi hupewa na Allah lililokuwa bora zaidi.

Ama swala za faradhi kuziswali katika swafu za mbele ni bora zaidi kwa kauli ya Mtume rehma na amani ziwe juu yake:((Bora ya swafu kwa wanaume ni swafu ya kwanza, na swafu ya shari kwao ni ya mwisho)).Ameipokea Imamu Muslim Allah amrehemu.

Na kauli yake Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake:

((Lau watu wangejua fadhila zinazo patikana katika Adhana na swafu ya kwanza, kisha hawakupata swafu ya kwanza isipokuwa kwa kupiga kura basi wangepiga kura)).

Ameupokea Imamu Bukhary na Muslim Allah awarehemu.

Na neno “Yastahimuu” maana yake ni: Kupiga kura.

Na fahamu ya kwamba swala moja katika Msikiti wa Mtume ni bora kuliko swala elfu moja katika Misikiti mingine ukitoa Msikiti mtukufu wa Makkah, kwani swala moja katika Msikiti mtukufu wa Makkah ni bora kuliko swala laki moja katika Misikiti mingine, amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake:((Swala moja katika Msikiti wangu huu ni bora kuliko swala elfu moja katika Misikiti mingine ukitoa Msikiti mtukufu wa Makkah, na swala moja katika Msikiti mtukufu wa Makkah ni bora kuliko swala laki moja katika Misikiti mingine)).(Imepokelewa na Ibni Maaja na Ahmad Allah awarehemu).

Kithirisha kusoma Qur’an na kumtaja Allah Mtukufu na kumshukuru na kumsifu na kutoa sadaka na kukaa itikafu katika Msikiti wa Mtume ikiwa itakuwa wepesi.

Ikiwa utapatwa na tatizo lolote katika mambo ya dini yako waulize wanachuoni miongoni mwao ni waalimu na mashekh wanao fundisha katika Msikiti wa Mtume kwa kutekeleza kauli ya Allah Mtukufu:(Waulizeni wanao jua ikiwa hamfahamu)[Al-Anbiya:7].

(Waulizeni wanao jua ikiwa hamfahamu)

[Al-Anbiya:7].

Au piga simu za (Idara ya mambo ya kutoa mwongozo kwa waulizaji) zilizo enezwa kwenye milango ya Maikiti na sehemu zingine, na utapata majibu ya kile kinacho kutatiza kuhusu ziara yako na ibada yako ya Hijja na Umra.

Jitahidi kuhudhuria Darsa mbali mbali zinazo tolewa na Mashekh wakubwa katika Msikiti mtukufu wa Mtume, ili ujifunze katika dini yako na uingie katika maneno ya Mtume rehma na amani ziwe juu yake inayosema:((Mwenye kuja katika Msikiti wangu huu basi atakuwa amekuja na jambo ili ajifunze au elimu ya kuwafundisha watu, huyo ana daraja la alie pigana jihadi katika dini ya Allah, na mwenye kuja kwa nia isiyokua hiyo atakuwa kama mtu aliekwenda kuangalia mizigo ya watu)). Maana yake atakuwa amepata hasara.Imepokelewa na Ibn Maajah, Ahmad na Al Haakim katika kitabu chake “Mustadrak” Allah awarehemu wote

((Mwenye kuja katika Msikiti wangu huu basi atakuwa amekuja na jambo ili ajifunze au elimu ya kuwafundisha watu, huyo ana daraja la alie pigana jihadi katika dini ya Allah, na mwenye kuja kwa nia isiyokua hiyo atakuwa kama mtu aliekwenda kuangalia mizigo ya watu)). Maana yake atakuwa amepata hasara.

Imepokelewa na Ibn Maajah, Ahmad na Al Haakim katika kitabu chake “Mustadrak” Allah awarehemu wote

Usisahau ndugu mgeni na unae tafuta elimu kutembelea Maktaba (Library) iliyopo katika Msikiti Mtukufu wa Mtume kwenye ukumbi mpana upande wa magaribi wa msikiti, katika eneo la upanuzi ulio fanywa na Mtumishi wa Misikiti mitukufu miwili Mfalme Fahdi Allah amrehemu, na anaetaka kufika hapo atapanda lifti namba (10) ya Umeme, ukifika hapo utapata mambo yatakayo kufaa.

Ndugu mgeni ikiwa ni katika watu wanao penda kusoma Makala na vitabu vilivyo andikwa na wanachuoni wa zamani (The manuscripts) vinavyo patikana kupitia mlango wa Othman Bin Afan radhi za Allah ziwe juu yake, na eneo hilo linapatikana mwisho wa upanuzi wa Msikiti wa mwanzo katikati ya Msikiti mtukufu wa Mtume.

Vile vile kuna Studio kwa ajili ya kurekodi sauti na video ambazo zinatumika katika kutoa muongozo, upande wa mlango namba (H17) -Mlango wa Omar Bin Khwatab -radhi za Allah ziwe juu yake- kwa upanuzi wa Mtumishi wa Misikiti mitukufu miwili Mfalme Fahdi -Allah amrehemu- studio hiyo inarekodi darsa mbalimbali na khutba na swala zote zinazo swaliwa katika Msikiti, na wanapewa bure wageni wote, wakileta CD mpya au USB au Hard disk, pia inapatikana Maktaba ya wanawake upande wanapo swalia wanawake mashariki ya msikiti mlango namba (24) na sehemu wanaposwalia wanawake magharibi mlango namba (16) na kuna maktaba ya sauti ya wanawake mlango namba (28).

Wakati wa swala Tangulia kwenye swafu na ujaze swafu ya kwanza kisha inayo fuatia, usiketi katika sehemu za kupita watu au mlangoni, au kwenye ngazi, ukifanya hivyo utakuwa umeziba njia za kupita na hilo litapelekea watu kuswali nje, ilihali ndani kuna nafasi.Bali jitahidi wewe na wenzako wanao swali kuunganisha swafu ili zinyooke na kuwaenea wenzako Msikitini.

Bali jitahidi wewe na wenzako wanao swali kuunganisha swafu ili zinyooke na kuwaenea wenzako Msikitini.

Ukitaka kuswali swafu ya kwanza au katika eneo la Raudhwa tukufu nenda Msikitini mapema usiende umechelewa kisha ukawaruka watu na kupita mbele ya wanao swali, na kusababisha msongamano wa watu, kufanya hivyo kunawaudhi wanao swali na hilo halifai.

Mtume rehma na amani ziwe juu yake alimuona mtu anawaruka watu Msikitini akitafuta sehemu ya kukaa siku ya ijumaa, na Mtume rehma na amani ziwe juu yake alikuwa anahutubia waislamu, akasitisha hutba na akamwambia:(Kaachini umewaudhi watu na wewe umechelewa kuja Msikitini)(Imepokelewa na Ibn Maajah na Ahmad Allah awarehemu)

(Kaachini umewaudhi watu na wewe umechelewa kuja Msikitini)

(Imepokelewa na Ibn Maajah na Ahmad Allah awarehemu)

yaani umewaudhi watu kwa kuwaruka na umechelewa kuja Msikitini, na ulitakiwa uje mapema kama unataka kuswali swafu za mbele.

Usipite mbele ya mtu anae swali, kwani Mtume rehma na amani ziwe juu yake amekataza kwa kusema:(Lau angejua mwenye kupita mbele ya mtu anae swali madhambi anayo pata, ingempasa asubiri kwa mda wa siku arobaini nibora kwake kuliko kupita mbele ya mtu anae swali).Amesema Abuu Nadhwar: Sijui kwamba alisema ni siku arobaini au miezi arobaini au miaka arobaini.Ameipokea Imamu Bukhary Allah amrehemu.Amesema Imamu Ibni Hajar Allah amrehemu katika kitabu “Fathul Baary” (1/585):”Kauli yake: (Ni bora angesimama arobaini): Maana yake ni kwamba anaye pita mbele ya mwenye kuswali lau angejua kiwango cha madhambi anayopata kwa kukupita kwake huko, basi ni bora angesimama kwa muda uliotajwa ili asipate madhambi hayo”.

(Lau angejua mwenye kupita mbele ya mtu anae swali madhambi anayo pata, ingempasa asubiri kwa mda wa siku arobaini nibora kwake kuliko kupita mbele ya mtu anae swali).

Amesema Abuu Nadhwar: Sijui kwamba alisema ni siku arobaini au miezi arobaini au miaka arobaini.

Ameipokea Imamu Bukhary Allah amrehemu.

Amesema Imamu Ibni Hajar Allah amrehemu katika kitabu “Fathul Baary” (1/585):

“Kauli yake: (Ni bora angesimama arobaini): Maana yake ni kwamba anaye pita mbele ya mwenye kuswali lau angejua kiwango cha madhambi anayopata kwa kukupita kwake huko, basi ni bora angesimama kwa muda uliotajwa ili asipate madhambi hayo”.

Jitahidi ndugu yangu mgeni kuwa msafi na kujitia manukato pamoja kuondoa harufu mbaya katika mwili na nguo, kwasababu hata Malaika wanachukia yale yanayo wachukiza wanadamu.

Hifadhi usafi wa Msikiti na maeneo yake, wala usiwaudhi ndugu zako wanaoswali katika Msikiti kwa kutema mate au makohozi katika sakafu ya Msikiti wa Mtume au maeneo mengine ya Msikiti, na unatakiwa uhisi utukufu wa sehemu hiyo, na ufahamu ya kwamba kutema mate Msikitini ni makosa kama alivyoeleza Mtume rehma na amani ziwe juu yake kwa kauli yake:((Kutema mate Msikitini ni makosa na kafara yake ni kuyafunika)).Ameupokea Imamu Bukhary na Muslim Allah awarehemu.

((Kutema mate Msikitini ni makosa na kafara yake ni kuyafunika)).

Ameupokea Imamu Bukhary na Muslim Allah awarehemu.

Usiwaache watoto wako wakacheza na kufanya upuuzi pamoja na kupiga kelele Msikitini, kwasababu mambo hayo yanapingana na adabu za Msikiti wa Mtume rehma na amani ziwe juu yake.

Epukana na sehemu zenye msongamano na ulazimiane na sehemu zenye nafasi katika Msikiti, na elewa ya kuwa ubora wa swala unapatikana sehemu yoyote katika Msikiti.

Ndugu yangu mgeni: Pumzika kidogo baada ya swala, na ufanye adhkaari zilizo thibiti baada ya swala, wala usiharakie kuswali Sunna baada ya swala ya faradhi na hasa katika nyakati na sehemu zenye msongamano, ili kuwapa fursa watu wenye dharura na wenye kutaka kutoka mapema waweze kutoka bila ya mashaka wala shida ya kupita mbele ya wanao swali.

Kuwa mtulivu na wala usikimbie na kusukuma watu wakati wa kuondoa kizuizi (pazia) linalo wekwa Raudhwa upande wa wanawake kwa ajili ya swala.

Usichukue Mas’hafu ukaondoka nayo kwasababu Mas’hafu hizo ni waqfu katika Msikiti Mtukufu wa Mtume.

Usiegemee kabati za Misahafu wala usiweke viatu pembezoni mwake wala usiziruke (wakati wa kutembea) kwa kuheshimu Kitabu cha Allah Mtukufu.

Ukiweka viatu vyako sehemu basi unatakiwa ujue mahala ulipo viweka (ili usisumbuke wakati wa kuvichukua).Sehem zote za kuwekea viatu zimewekewa namba pembeni au juu yake, unatakiwa kujua namba ya sehemu ulipoweka viatu vyako ili uweze kuchukua viatu vyako kwa wepesi pindi ukirudi.

Sehem zote za kuwekea viatu zimewekewa namba pembeni au juu yake, unatakiwa kujua namba ya sehemu ulipoweka viatu vyako ili uweze kuchukua viatu vyako kwa wepesi pindi ukirudi.

Ndugu yangu mgeni tambua ya kwamba Msikiti wa Mtume pamoja na Misikiti mingine imejengwa kwa ajili ya ibada, basi usiifanye kuwa ni sehemu ya kulala au kuombaomba au sehemu ya kuimba.

Usiyatumie kwa udhu mambomba yanayotoa maji ya zamzam yaliyopo Msikitini au plastiki zilizojazwa maji ya zamzam kwa ajili ya kunywa, wala usitumie zulia la Msikiti kama mto wa kulalia au kitu cha kujifunika.

Jiepushe na kutandika vitu vya kukali katiika maeneo ya Msikiti mtukufu wa Mtume.

Imekatazwa kuvuta sigara katika maeneo ya Msikiti wa Mtume na viunga vyake, na mtu mwenye mtihani wa kuvuta sigara basi ajitahidi kujinyenyekeza kwa Allah katika Msikiti wa Mtume rehma na amani ziwe juu yake, ili Allah Mtukufu aweze kumjaalia aache sigara, na atambue ya kuwa Wanachuoni wametoa fatwa kwamba kuuza na kuvuta sigara ni haramu. Na ajue kuwa mwenye kuvuta sigara anapata madhambi, ewe ndugu yangu mgeni hakika umekuja kuzuru Msikiti wa Mtume ili kujizidishia mambo mema na ya kheri, basi jihadhari sana na madhambi.

Milango yote ya Msikiti Mtukufu wa Mtume imepewa majina na namba, jitahidi kujua majina na namba ya mlango ulio ingilia ili utoke kupitia mlango huo.

Ukiona msongamano kwenye mlango wa Msikiti jitahidi kukaa Msikitini kidogo mpaka msongamano wa watu upungue.

Usisahau wakati wa kutoka Msikitini tanguliza mguu wa kushoto na kusoma dua ifuatayo:(Bismillah, Allahuma swali wasalim ala Muhammad, Allahuma ighfir liy dhunuubiy waftah liy ab’waba fadhilika). (Kwajina la Allah ewe Allah mteremshie rehma Mtume, ewe Allah nisamehe madhambi yangu na unifungulie milango ya fadhila zako).(Imepokelewa Maimamu wa hadithi kama: Tirmidhiy na Ibn Maajah, na Ahmad, na hadithi hii ina ushahidi wa hadithi nyingine katika kitabu cha Swahihi Muslim, Allah awarehemu wote).

(Bismillah, Allahuma swali wasalim ala Muhammad, Allahuma ighfir liy dhunuubiy waftah liy ab’waba fadhilika). (Kwajina la Allah ewe Allah mteremshie rehma Mtume, ewe Allah nisamehe madhambi yangu na unifungulie milango ya fadhila zako).

(Imepokelewa Maimamu wa hadithi kama: Tirmidhiy na Ibn Maajah, na Ahmad, na hadithi hii ina ushahidi wa hadithi nyingine katika kitabu cha Swahihi Muslim, Allah awarehemu wote).

Tunakunasihi uchukue kadi ya hoteli ulio fikia ili uitumie ikiwa utapotea na kuto kupajua ulipo fikia.

Ikiwa kuna mgonjwa ambae yuko Msikitini na anahitaji kupelekwa Hospitali, fanya haraka kutoa taarifa kwa walinzi walioko katika milango ya Msikiti, au yeyote alie beba radio call, na wafanya kazi wengine.

Eneo la juu la Msikiti mtukufu wa Mtume linafunguliwa kila siku ya Ijumaa na nyakati za Hijja linafunguliwa katika nyakati zote za swala, ikiwa utaona kuna msongamano wa watu basi panda juu utapata nafasi nzuri ya kuswali.

Kuna vigari vya kubebea wagonjwa na wazee wanapewa wenye kuhitaji, vinatolewa na Idara ya Msikiti mtukufu wa Mtume mlango namba (8) upande wa magharibi wa msikiti, kwa ajili ya kuwabeba wagonjwa au wazee kutoka Msikitini kwenda kwenye makazi yao au kwenye magari yao kwa muda wote wa kuwepo katika Msikiti mtukufu wa Mtume.

Usimtangulie Imamu wakati wa kuswali katika wakati wa msongamano wa watu katika viwanja vya mbele upande wa Kibla, ili kuepuka tofauti za wanachuoni kuhusu kufaa au kuto kufaa kuswali mahala hapo.

Jitahidi kufuata miongozo na maelekezo ya wasimamizi waliopo Msikitini, ambao wamewekwa kwa ajili ya kukuhudumia na kuhakikisha wanakurahisishia ibada yako.

Jitahidi kunyenyekea sana na kuomba dua pamoja na kumuahidi Allah kwa kufanya toba iliyo ya kweli, na tambua ya kuwa adabu ya kweli kwa Allah Mtukufu ni kumpenda na kumtukuza na kumtakasia dini, na adabu ya kweli kwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake ni kufuata Sunna na zake na mwongozo wake, na kuiga matendo ya Maswahaba wake baada yake, pamoja na kumheshimu Mtume rehma na amani ziwe juu yake hata baada ya kufa kwake.

Na Mwisho: Nakuusia ndugu yangu mgeni (kumswalia) kumtakia rehma na amani sana Mtume wetu na bwana wetu Muhammad rehma na amani ziwe juu yake, imekuja kutoka kwa Amru bnil A’swi radhi za Allah ziwe juu yake, ya kwamba alimsikia Mtume rehma na amani ziwe juu yake akisema:((Mwenye kunitakia rehma mara moja basi Allah humtakia rehma mtu huyo mara kumi)).Ameipokea Imamu Muslim na wengine.

((Mwenye kunitakia rehma mara moja basi Allah humtakia rehma mtu huyo mara kumi)).

Ameipokea Imamu Muslim na wengine.

Na uzidishe kufanya adhkaari zilizo thibiti pamoja na kujinyenyekeza kwa Allah na kuelekea kwake, kwasababu upo katika sehemu ambayo dua zako ni haraka sana kujibiwa, wala usisahau katika dua zako kuwaombea wazazi wako, mke na watoto wako na ndugu zako na waislamu duniani kote.

Na rehma na amani za Allah ziwe juu ya Mtume wetu Muhammad na ali zake na Maswahaba zake wote.

To read more about the Kuutembelea Msikiti Ntukufu Wa Mtume book Click the download button below to get it for free

or

Report broken link
Support this Website


for websites

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *