Skip to content
Home » Mukhtasari Wa Maneno Katika Nguzo Za Uislamu pdf

Mukhtasari Wa Maneno Katika Nguzo Za Uislamu pdf

MUKHTASARI WA MANENO KATIKA NGUZO ZA UISLAMU
  • Book Title:
 Mukhtasari Wa Maneno Katika Nguzo Za Uislamu
  • Book Author:
Abdallah Bin Muhammad Bin Ahmad Al Twayyaar
  • Total Pages
248
  • Book Views:

Loading

  • Click for the  
PDF Direct Download Link
  • Get HardCover  
Click for Hard Copy from Amazon

MUKHTASARI WA MANENO KATIKA NGUZO ZA UISLAMU – Sampuli

Maana Ya Udhu: -( MUKHTASARI WA MANENO KATIKA NGUZO ZA UISLAMU PDF)

Ni kutumia maji safi katika kusafisha viungo vinne : (Uso, mikono miwili, kichwa na miguu miwili), kwa namna maalumu iliyoelekezwa na Qur’an na Sunna.

Dalili Yake Kutoka Katika Qur’an :

Amesema Allaah mtukufu :

{Enyi Mlioamini! Mnaposimama kwa ajili ya Sala, basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni. Na mkiwa na janaba basi ogeni}. [Al Maida: 6].

Na Katika Sunna :

Amesema Abu Hurayra Allaah amridhiye kuwa: Mtume Rehema na Amani zimshukie amesema: (Haikubaliki sala ya mtu yoyote anapojichafua mpaka atawadhe).45

Fadhila Za Udhu:

Hakika udhu una fadhila nyingi.Tutazitaja baadhi yake ili kubainisha fadhila zake.

Amesema Allaah mtukufu katika kubainisha fadhila zake: {Allaah hapendi kukutieni katika taabu, bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake juu yenu ili mpate kushukuru}. [Al Maida: 6].

Ama dalili kutoka katika Sunnani nyingi sana, miongoni mwa hazo ni:

1. Kutoka kwa Abu Hurayra Allaah amridhiye ame-sema: Nilimsikia Mtume Rehema na Amani zimshukie akisema: (Hakika umati wangu wataitwa siku ya kiama hali ya kuwa wakiwa ni weupe waking’aa kutokana na athari ya udhu, basi atakayeweza miongoni mwenu kuzidisha mng’ao wake na afanye hivyo).46

2. Kutoka kwa Othman bin Affaan Allaah amridhiye amesema: Amesema Mtume Rehema na Amani zimshukie: (Yeyote atakayetawadha, na akafanya vizuri udhu wake, basi madhambi yake hutoka katika mwili wake mpaka chini ya kucha zake).47

3. Kutoka kwa Abu Hurayra Allaah amridhiye ame-sema: Amesema Mtume Rehema na Amani zimshukie: (Anapotawadha mja Mwislamu au Muumini akaosha uso wake, hutoka katika uso wake kila dhambi iliyoangali-wa na macho yake pamoja na maji au pamoja na tone la mwisho la maji, na anapoosha mikono yake, basi hutoka madhambi yote yaliyofanywa na mikono hiyo pamoja na maji au pamoja na tone la mwisho la maji, na anapoosha miguu yake, basi hutoka madhambi yake yote yaliyotem-belewa na miguu hiyo pamoja na maji au pamoja na tone la mwisho la maji, mpaka anapomaliza huwa ni msafi ku-tokana na madhambi).48

4. Kutoka kwa Omar bin Khatwabi (Allaah amrid-hiye) amesema: Amesema Mtume Rehema na Amani zimshukie: (Hakuna yeyote miongoni mwenu anayet-awadha, akaufanya vizuri udhu wake), kisha akasema baada yake: (Ninashuhudia kuwa hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allaah peke yake asiye na mshirika, na ninashuhudia kuwa hakika Muhammad ni Mja wake na Mtume wake, ispokuwa mtu huyo hufun-guliwa milango minane ya pepo, aingie kwenye mlango wowote autakao).49Na akaongezea Tirmidhiy kuwa : ki-sha akasema Mtu huyo: (Ewe Allaah ninakuomba unijaa-lie miongoni mwa wenye kutubu, na unijaalie miongoni mwa wenye kujisafisha).50

Faradhi Za Udhu:

Udhu una nguzo sita ambazo ni:

  1. Kuosha uso mara moja tu, kuanzia juu ya paji la uso mpaka mwisho wa chini ya kidevu, na kuanzia kwenye sikio mpaka sikio lingine, kutokana na ushahidi wa kauli ya Allaah: {Osheni nyuso zenu}.[Al Maida: 6]. 

Na hapo inaingia katika hukumu ya uso kusukutua mdomo na kusafisha pua, kutokana na viungo hivyo kuz-ingatiwa ni katika uso, kama alivyosema Mtume Rehema na Amani zimshukie : (Anapotawadha mmoja wenu basi aweke mdomoni mwake maji kisha na ayapenge puani).51

2. Kuosha mikono miwili mpaka vifundoni, kwa ushahidi wa kauli ya Allaah: {Na ( osheni ) mikono yenu mpaka vifundoni}. [Al Maida: 6].

3. Kupaka maji kichwani kuanzia mwanzo wa paji la uso mpaka kisogoni, kwa ushahidi wa kauli ya Allaah: {Na mpake vichwa vyenu}. [Al Maida: 6].

4. Kuosha miguu miwili mpaka vifundoni, kwa ushahidi wa kauli ya Allaah: {Na osheni miguu yenu mpaka vifundoni}. [Al Maida: 6].

5. Utaratibu: Nao ni kwa kuanzia kuosha uso, kisha kuosha mikono miwili, kisha kupaka kichwa, kisha kuosha miguu miwili, kwa sababu ya kupatikana utaratibu huo katika amri ya Allaah.

6. Kufululiza: Kwa maana kufanya matendo ya udhu kwa wakati mmoja bila kuachanisha kwa muda mrefu. Ispokuwa kama itakuwa hivyo kidogo tu haina madhara. Siyo kuachanisha kipindi kirefu mpaka kiungo kimoja kikauke maji.

Sunna Za Udhu:

1.         Kupiga mswaki.

2.         Kuanza kwa kusema “Bismi LLah” (Kwa jina la Allaah).

3. Kuanza udhu kwa kuosha viganja viwili mara tatu. Lakini ikiwa mtu ametoka kulala, anawajibika kuviosha viganja vyake kwanza mara tatu kabla ya kuviingiza ka-tika maji ya udhu, kama alivyosema Mtume Rehema na Amani zimshukie: (Atakapoamka mmoja wenu usingizini basi aoshe viganja vyake mara tatu kabla ya kuviingiza katika chombo, kwani yeye hajui mikono yake ililala mae-neo gani).52

4. Kuanza kusukutua mdomoni na kupenga maji puani

kabla  ya  kuosha  uso  pamoja  na  kupandisha  sana  maji mdomoni kwa asiyekuwa Mfungaji.

5. Kuesua ndevu nyingi ili maji yaingie ndani yake.

6. Kuanza upande wa kulia, kwa kuosha viungo vya kulia kwanza kisha vya kushoto.

7. Kuomba dua baada ya kumaliza udhu.

8. Kuswali rakaa mbili baada ya udhu, inaitwa Sunna ya udhu.

Yasiyo Pendeza (Yasiyofaa) Katika Udhu:

1. Kutawadha katika sehemu yenye najisi ili kuepusha isimrukie.

2. Kuzidisha zaidi ya mara tatu katika kutawadha.

3. Kufanya uharibifu wa maji (israfu).

4. Kuacha sunna moja au zaidi, miongoni mwa sunna za udhu, kwa sababu hapati malipo.

5. Kutawadha maji yaliyoachwa na Mwanamke (Yale maji aliyokwishatawadhia yakabakia katika chombo).

Namna Ya Kutawadha:

Udhu una namna mbili:

Ya Kwanza: Udhu unaotosheleza:

Nao ni kuanza kwa nia, kisha kusema: “Bismi LLah”, kisha kusukutua na kupenga maji puani, kisha kuosha uso, kisha kuosha mikono miwili mpaka vifundoni, kisha kupaka kichwa pamoja na masikio, kisha kuosha miguuni mpaka vifundoni.

Kuosha viungo vyote hivi mara moja moja tu.Namna hii inatosheleza na udhu ni sahihi.

Ya Pili: Udhu ulio kamili:

Nao ni kuanza kwa nia, kisha kusema: “Bismi LLah”,na kuosha viganja viwili mara tatu, kisha kusukutua mdomoni na kupenga maji puani mara tatu kwa michoto mitatu, kisha kuosha uso mara tatu, kisha kuosha mkono wa kulia mpaka kifundoni mara tatu, kisha kuosha mkono wa kushoto mpaka kifundoni mara tatu, kisha kupaka kichwani mara moja kuanzia mwanzo wa kichwa mpaka kisogoni na kurudishia mpaka mwanzoni mwa kichwa tena na kuingiza vidole vyake ndani ya matundu ya masikio kwa vidole gumba nje yake na vidole shahada ndani yake, kisha kuosha mguu wa kulia pamoja na muundi mara tatu, kisha kuosha mguu wa kushoto pamoja na muundi mara tatu.Kisha akimaliza hivyo vyote aseme: “Ninashuhdia kuwa hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allaah peke yake asiye na mshirika, na ninashuhudia kuwa hakika Muhammad ni Mja wake na Mtume wake”.

To read more about the Mukhtasari Wa Maneno Katika Nguzo Za Uislamu book Click the download button below to get it for free

or

Report broken link
Support this Website


for websites

1 thought on “Mukhtasari Wa Maneno Katika Nguzo Za Uislamu pdf”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *