Skip to content
Home » Tafsir Surat Yusuf in Swahili Language pdf download

Tafsir Surat Yusuf in Swahili Language pdf download

TAFSIR SURAT YUSUF IN SWAHILI LANGUAGE
  • Book Title:
 Tafsir Surat Yusuf In Swahili Language
  • Book Author:
AL MUSTAKSHIF ABU MANAL DANAH
  • Total Pages
315
  • Book Views:

Loading

  • Click for the  
PDF Direct Download Link
  • Get HardCover  
Click for Hard Copy from Amazon

TAFSIR SURAT YUSUF IN SWAHILI LANGUAGE by Al Mustakshif Abu Manal Danah تفسيرسورة يوسف

sampuli – TAFSIR SURAT YUSUF IN SWAHILI LANGUAGE

 إِذْ قَالَ يُوسُفُ لِأَبِيهِ يَا أَبَتِ إِنِّي رَأَيْتُ أَحَدَ عَشَرَ كَوْكَبًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ رَأَيْتُهُمْ لِي سَاجِدِينَ.

 السورة ورقم الآية: يوسف (4).

Idh qala yoosufu li-abeehi ya abati innee raaytu ahada AAashara kawkaban waalshshamsa waalqamara raaytuhum lee sajideena (Surat Yusuf 12:4)

Tafsir: Aliposema Yusuf kumwambia Baba yake: Ewe Baba yangu Hakika Mimi Nimeona Kumi na Moja Nyota Na Jua na Mwezi nimeziona zikinisujudia.

Naam aya yetu imetumia neno Kawkaban ambalo kwa Kilugha ya Kiarabu basi neno Kawkaba hua ni lenye Kumaanisha Kung’ara au Kumeremeta ambayo hua ni hali ya kiwakilishi cha Sifa. Ambapo pale neno Kawkaba linapotumika katika hali ya Jina basi linamaanisha Nyota, Sayari, Weupe wa Jicho, Tone la Umande, Upanga Mweupe, Sehemu ya ardhi yenye rangi tofauti na rangi ya asili ya sehemu nyengine zilizozunguka eneo hilo, Uwa la Bustanini na pia hua linamaanisha Kijana Mwanamme mwenye Sura ya Kuvutia na Kupendeza. 

Na ukweli ni kua tunapozungumzia juu ya Nyota au Sayari basi Qur’an imetumia maneno tofauti ikiwemo Masaabih, Nujuum, Kawakib, Buruj n.k ambapo hua kuna tofauti ndogo baina yake kwani zote hua ni zenye Kung’ara. Ila tunapozungumzia kwa upande wa Kisayansi basi bila ya shaka hua kuna utofauti baina yao kwa mfano:

Kawkab hua ni Sayari au Nyota yeyote ambayo haina muangaza wake wa asili na hivyo kung’ara kwake hua kunategemeana na Muangaza wa Jua na hivyo hua hazimeremeti.

Ambapo Najmun ambapo wingi wake hua Nujum basi hua ni Sayari au Nyota ambayo hua ina Muangaza wake wa asili na hivyo hua ni yenye kungara bila kutegemea Muangaza wa Jua na hivyo hua ni zenye Kumeremeta, na hua ni zenye asili ya kuchomoza kama linavyochomoza Jua kwani neno Nujum pia hua ni lenye kumaanisha Kuchomoza, Kuanza, Kukamilisha au Kupitiliza.

Hivyo ili kufaham zaid basi na tuangalie mfano ufuatao, ambapo anasema Allah Subhanah wa Ta’ala katika Qur’an:

To read more about the Tafsir Surat Yusuf In Swahili Language book Click the download button below to get it for free

or

Report broken link
Support this Website


for websites

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *