Skip to content
Home » WENYE AZMA THABIT ZAIDI MIONGONI MWA MITUME pdf

WENYE AZMA THABIT ZAIDI MIONGONI MWA MITUME pdf

UULU AL AZMI MINA ALRRUSUL AL JUZUI AL AWWAL – SWAHILI

WENYE AZMA THABIT ZAIDI MIONGONI MWA MITUME
  • Book Title:
 Wenye Azma Thabit Zaidi Miongoni Mwa Mitume
  • Book Author:
AL MUSTAKSHIF ABU MANAL DANAH
  • Total Pages
965
  • Book Views:

Loading

  • Click for the  
PDF Direct Download Link
  • Get HardCover  
Click for Hard Copy from Amazon

WENYE AZMA THABIT ZAIDI MIONGONI MWA MITUME – Sampuli

WENYE AZMA THABIT ZAIDI MIONGONI MWA MITUME

(فَاصْبِرْ كَمَا صَبَرَ أُولُو الْعَزْمِ مِنَ الرُّسُلِ)

Faisbir kama sabara oloo alAAazmi mina alrrusuli (Surat Al Ahqaf 46:35)

Tafsir: Hivyo kua na Subira kama walivyokua na Subira Ulul A’zmi miongoni mwa Mitume.

Neno A’zmi linatokana na neno la Kiarabu A’zama ambalo hua ni lenye kumaanisha Azma, Amuzi lisilotenguka wala kupingika, Kusudio, Lengo au Msimamo thabit usiotetereka na hivyo kua na thamani ambayo inapelekea kusudio husika kutoachika njiani na hivyo hua ni lenye kufuatiliwa au kutekelezwa hadi likamilie.

Hivyo Uluu al A’zmi Mina Al Rusul hua ni Mitume na Manabii ambao walikabiliwa na mitihani mikubwa sana yenye kuvunja Moyo mara kadhaa katika kutekeleza kazi yao ya kuwaongoza watu na kueneza ujumbe wa Allah, lakini hata hivyo hawakuvunjika moyo bali waliendelea kufanya jithada za kueneza ujumbe huo kwa subira na ustahmilivu mkubwa sana.

Allah Subhanahu wa Ta’ala amewataja Ulul A’zmi katika sehemu mbili ndani ya Qurán ambapo ni katika Surat Al-Ahzab (33:7) na Surat Ash-Shuara (42:13).

Ambapo katika Surat Al Ahzab (33:7) Allah Subhanah wa Ta’ala amesema kua:

(وَإِذْ أَخَذْنَا مِنَ النَّبِيِّينَ مِيثَاقَهُمْ وَمِنكَ وَمِن نُّوحٍ وَإِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ۖ وَأَخَذْنَا مِنْهُم مِّيثَاقًا غَلِيظًا)

Wa-idh akhadhna mina alnnabiyyeena meethaqahum waminka wamin Nuuhin wa-Ibraheema waMuusa waAAeesa ibni Maryama waakhadhna minhum meethaqan ghaleedhan (Surat Al Ahzab 33:7)

Tafsir: Na kumbuka wakati tulipochukua kutoka kwa Manabii ahadi zao, na kutoka kwako wewe (Muhammad) na Nuh, na Ibrahim, na Musa na Isa Ibn Maryam. Na tumechukua kutoka kwao ahadi madhubuti.

Na pale aliposema katika Surat Ash Shuara:

(شَرَعَ لَكُم مِّنَ الدِّينِ مَا وَصَّىٰ بِهِ نُوحًا وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَمَا وَصَّيْنَا بِهِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَىٰ ۖ أَنْ أَقِيمُوا الدِّينَ وَلَا تَتَفَرَّقُوا فِيهِ ۚ كَبُرَ عَلَى الْمُشْرِكِينَ مَا تَدْعُوهُمْ إِلَيْهِ ۚ اللَّهُ يَجْتَبِي إِلَيْهِ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي إِلَيْهِ مَن يُنِيبُ)

SharaAAa lakum mina alddeeni ma wassa bihi Noohan waalladhee awhayna ilayka wama wassayna bihi Ibraheema wamoosa waAAeesa an aqeemoo alddeena wala tatafarraqoo feehi kabura AAala almushrikeena ma tadAAoohum ilayhi Allahu yajtabee ilayhi man yashao wayahdee ilayhi man yuneebu(Surat Ash Shuara 42:13)

Tafsir: Tumekushushieni Sharia katika dini kama vile tulivyomuusia Nuh. Na vile ambavyo tulivyokushushia wewe na kama tulivyomuusia Ibrahim, na Musa, na Isa kuwaambia msimamishe Dini wala msisababishe mgawanyiko ndani yake. Wasichoweza kukistahmilia Makafiri ni kuwaita kwako katika njia ya Allah. Allah humchagua amtakae na humuelekeza katika upande wake yule anaemgeukia yeye kwa ustahmilivu na utiifu.

Na igawa Wanazuoni wanakubaliana kua Mitume na Manabii waliotajwa kwa majina waliotajwa kwenye aya hizi mbili yaani Nabii Nuh, Nabii Ibrahim, Nabii Musa, Nabii Isa na Nabii Muhammad tu Salallahu A’layhi wa Salam, lakini kwa upande wa Imam Abu Muh basi yeye anasema kuhusiana na aya isemayo:

(فَاصْبِرْ كَمَا صَبَرَ أُولُو الْعَزْمِ مِنَ الرُّسُلِ)

Faisbir kama sabara oloo alAAazmi mina alrrusuli (Surat Al Ahqaf 46:35)

Tafsir: Hivyo kua na Subira kama walivyokua na Subira Ulul A’zmi miongoni mwa Mitume.

Kua: ‘Aya hii inamaanisha kusema kua: ‘Kua na Subra kama wenye (Sabr) Subra miongoni mwa watu wenye maarifa (Ahl Al Maarifa) kama vile walivyokua wale wenye maazimio thabiti (Uluu al Azmi) miongoni mwa Mitume walioonesha Subra, Subra ambayo ni moja kati ya njia za kua na Maridhio (Ridhaa) na Kujisalimisha (Taslima) bila ya kua na masikitiko (Shakwa) au kukosa ustahmilivu (Jaza). 

Nabii Ibrahim alipewa mtihani wa kuingizwa ndani ya tanuri la moto na mtihani wa kumtoa Muhanga mtoto wake, lakini alipokea Mitihani hio kwa maridhio na kujisalimisha, Nabii Nuh alipewa mtihani  wa kutokukubaliwa na watu wake lakini nae akawa ni mwenye Subira (Sabara), wakati Nabii Yunus alipewa mtihani wa kuishi ndani ya tumbo la Nyangumi lakini akawa ni mwenye kumkumbuka Mola wake, na kuomba hifadhi kutoka kwake, Nabii Yusuf alipewa mtihani wa kutumbukizwa Kisimani na kufugwa Jela lakini hakutetereka. Nabi Yaqub alipewa mtihani wa kupoteza macho yake na kupoteza mtoto wake, lakini alimlamikia Mola wake na hakulalamika kwa Ibn Adam yeyote. Kuna Mitume 12 ambao Sala na Salam za Allah ziwe juu yao, waliokua na Subra na ustahmilivu juu ya mitihani yao iliyowafika na hivyo kua ni wenye kujulikana kama Wenye Misimamo Thabiti (Ulu al Azmi) miongoni mwa Mitume, lakini Allah Subhanah wa Taála ni mwenye kujua zaidi’’

Ingawa Nabii Adam alikua ni mtu wa mwanzo na Nabii wa mwanzo lakini Nabii Idris ambae alikua anatoka katika kizazi cha tano kutoka kwa Nabii Adam alikua ni mtu wa mwanzo kupewa Utume baada ya Nabii Adam. Nabii Idris alizaliwa na alikulia katika mji wa Babylon ambao uliokuwepo katika maeneo ya Iraq.

Katika wakati wa uhai wake, Nabii Idris alijaribu kuwarudisha watu wake wale waliopotoshwa na Iblis na kutolewa kutoka katika njia ya haki lakini ni wachache sana waliomsikiliza na wengi waliobakia miongoni mwao walimpinga na kumkataa. Hivyo akaendelea kuwausia mema na kuwakataza mabaya na baadae akaamua kuhama na wale waliomkubali na kuhamia katika maeneo ya Ardhi ya Misri ambako alikaa huko hadi kufariki kwake. Qurán inasema kuhusiana na Nabii Idris kua:

(وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ إِدْرِيسَ ۚ إِنَّهُ كَانَ صِدِّيقًا نَّبِيًّا (56) وَرَفَعْنَاهُ مَكَانًا عَلِيًّا (57) أُولَٰئِكَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ مِن ذُرِّيَّةِ آدَمَ وَمِمَّنْ حَمَلْنَا مَعَ نُوحٍ وَمِن ذُرِّيَّةِ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْرَائِيلَ وَمِمَّنْ هَدَيْنَا وَاجْتَبَيْنَا ۚ إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُ الرَّحْمَٰنِ خَرُّوا سُجَّدًا وَبُكِيًّا ۩)

Waodhdkur fee alkitabi idreesa innahu kana siddeeqan nabiyyan; WarafaAAnahu makanan AAaliyyan ; Ola-ika alladheena anAAama Allahu AAalayhim mina alnnabiyyeena min dhurriyyati adama wamimman hamalna maAAa noohin wamin dhurriyyati ibraheema wa-isra-eela wamimman hadayna waijtabayna idha tutla AAal jadan wabukiyyan  (Surat Maryam 19:56-58).

Tafsir: Na ametajwa katika Kitabu (Qurán) Idris. Hakika yeye alikua ni mtu mkweli na ni Nabii. Tulimnyanyua katika darja ya juu. Hawa ndio wale ambao Allah Subhanah wa Ta’ala amewapa fadhila zake miongoni mwa Mitume, waliotokana na kizazi cha Adam, na wale uliowabeba (katika Safina) pamoja na Nuh, na kizazi cha Ibrahim, na Israil (Nabii Yaqub) na miongoni mwa wale ambao tumewaongoza na kuwachagua. Wanaposomewa Aya za mwingi wa Rehma (Allah Subhanah wa Taála) basi huanguka chini huku wakiwa katika hali ya Kusjudu huku wakibubujikwa na machozi.

Naam, aya hizi za Surat Maryam 19:56-58 ni aya ambazo zinathibitisha kua Nabii Idris alikuja kabla ya kuja Nabii Nuh, kwa sababu aya imeanza na kumuelezea Nabii Idrisa na kumjumuisha kua ni miongoni mwa waliopewa fadhila miongoni mwa kizazi cha Nabii Adam, kisha vikatajwa vizazi vya Nabii Nuh, Nabii Ibrahim na Nabii Yaqub.

Baada ya kufariki Nabii Nabii Idris A’layhi Salaam, ilipita miaka mingi sana na kama kawaida yake Iblis akazidi kuongeza jitihada zake za kuwapotosha watu na watu hao wakaanza kutengeneza masanamu na kuyaabudia na kuamini kua yalikua na uwezo wa kuwanufaisha na kuwalinda na mengi. Anasema Imam Ibn Jarir kua: ‘Watu wema walioishi baina ya Adam na Nuh na wale waliokua wakiwafuata walitengeneza masanamu yao na kusema: ‘Ikiwa tutafanya Masanamu yao, basi itapendeza zaid katika kufanya Ibada zetu na pia itatukumbusha kuhusiana na wao’ hivyo wakatengeneza Masanamu, na baada ya kufariki wale waliotengeneza Masanamu hayo, basi Iblis akawashawishi waliofuatia kwa kuwaambia: ‘Mababu zenu walikua wakiwaabudu hawa na kupitia katika Ibada zao hizo walikua wakipata mvua.’ hivyo nao wakawa wanayaabudu.’’ 

Na waliendelea kufanya hivyo hadi pale Allah Subhanah wa Ta’ala alipoamua kumtuma Nabii wa tatu, ambae ni Nabii Nuh Alayhi Salatu wa Salam.

To read more about the Wenye Azma Thabit Zaidi Miongoni Mwa Mitume book Click the download button below to get it for free

or

Report broken link
Support this Website


for websites

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *