
| Zawadi Ya Msomaji Katika Kufahamu Maneno Ya Manani |
| Ahmad Khalil Shahin, Seif Abubakar Ruga |
| 353 |
| |
| PDF Direct Download Link |
| Click for Hard Copy from Amazon |
Microsoft Word – Al-Hajj Al-Mabroor.doc
ZAWADI YA MSOMAJI KATIKA KUFAHAMU MANENO YA MANANI – Sampuli
Sura ya Al-Baqara – (ZAWADI YA MSOMAJI KATIKA KUFAHAMU MANENO YA MANANI)
Sura hii imeteremshwa Madina, isipokuwa Aya moja tu ya 281, Aya hii imeshuka katika Hijja ya mwisho ya Mtume “Hijjat Al-Wadaai” Na hii ndio Sura ya mwanzo kushuka katika Sura za Madina. Idadi za Aya zake ni (286) kwa mujibu wa Mtazamo wa Wanazuoni wa kufa.”
Yaliyomo Katika Ubora wa Sura ya Al-Baqara
Hadithi iliyopokewa kutoka kwa Abu Umama Al-Bahili dic del sis, amesema: Nimemsikia Mtume plugule all olo anasema:
“اقرأوا سورة البقرة، فإن أخذها بركة، وتركها حسرة، ولا تستطيعها البطلة”
“Someni Sura Al-Baqara hakika katika kuisoma kuna Baraka na kuiacha kuna hasara, na wala kinga yake hawaivunji wachawi”l0
Hadithi iliyopokewa na Abdillah bin Masudi amesema: Mtume wa Allah amesema
“من قرأ بالآيتين من آخر سورة البقرة في ليلة كفتاه”
“Na mwenye kusoma Aya mbili mwisho wa Sura ya Al-Baqara katika usiku mmoja tu humtosheleza Aya hizo.”!?
Madhumuni ya Sura
Sura inazungumzia sifa za msingi za wacha-mungu na malipo yao kwa Allah Gothes, kadhalika Sura inazungumzia makafiri na wanafiki, na mwanzo wa kuumba, na uumbwaji wa Adamu na amri ya kumsujudia Adamu na kukataa Ibilisi kumsujudia. Vile vile Sura inazungumzia habari ya Wana wa Israili na kuvunja kwao ahadi. Sura pia inahadithia kuhusu Ibrahim na mwanawe Ismaili na ujenzi wa nyumba tukufu Al-Ka’aba, na ubadilishaji wa Qibla kutoka Msikiti wa Al-Aqsa na kuelekea Msikiti Mtakatifu wa Makka.
Kadhalika, Sura inazungumzia Ibada tukufu ya Hijja na Umra, na uhakika wa wema na aina zake. Vilevile, Sura inazungumzia kuhusu Funga, Wasia, Swali kuhusu habari ya miezi miandamo, pombe, kamari, viapo kwa ujumla wake na kiapo cha talaka, kisa cha Wana wa Israili pamoja na Mtume aliyetumwa kwao, kisa cha Nabii Ibrahim pamoja na mtu aliyejadiliana naye kuhusu Mola wake Mlezi, Aya ya Al-Kursi, ria na hukumu zake na Aya za kuandikishiana wakati wa kudaiana pamoja na Hukumu zake.
Sababu ya Kushuka Aya
Kuna sababu (16) za kushuka kwa Aya katika Sura hii.
- Allah Amesema:
قُلْ مَن كَانَ عَدُوًّا لِّجِبْرِيلَ فَإِنَّهُ نَزَّلَهُ عَلَىٰ قَلْبِكَ بِإِذْنِ اللَّهِ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ (97) مَن كَانَ عَدُوًّا لِّلَّهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَرُسُلِهِ وَجِبْرِيلَ وَمِيكَالَ فَإِنَّ اللَّهَ عَدُوٌّ لِّلْكَافِرِينَ
“Sema: Aliyekuwa ni adui wa Jibril, basi huyo ndiye aliyeiteremsha Qur’ani moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, inayothibitisha yaliyokuwa kabla yake, na ni uwongofu na bishara njema kwa Waumini. Aliyekuwa adui wa Mwenyezi Mungu Na Malaika Wake na Mitume Wake na Jibril na Mikail, basi hakika Mwenyezi Mungu ni adui wa makafiri.” (2:97 – 98)
Hadithi iliyonukuliwa na Bukhari kutoka kwa Anasi bin Malik dis al sis amesema: Abdillah bin Salami alisikia kuja kwa Mtume wa Allah ale al to plug akiwa katika ardhi yake akishughulika. Hivyo basi akamuendea Mtume akasema: Hakika mimi nitakuuliza mambo matatu hawezi kuyajibu mambo hayo ila Mtume tu: Ni zipi dalili na ishara za awali za Kiama?. Na ni kipi chakula cha awali kwa watu wa peponi?. Na ni kitu gani kinachomfanya mtoto afanane na baba yake au mama yake? Mtume akasema
أخبرني به جبریل آنفا”
“Majibu ya maswali hayo amenifahamisha Jibril sasa hivi.”
Akauliza, “Jibril?’ Mtume akasema:
“Ndio”
Akasema: “Huyu miongoni mwa malaika ni adui wa Mayahudi.’ Mtume dil to
:akasoma Aya hii
قُلْ مَن كَانَ عَدُوًّا لِّجِبْرِيلَ فَإِنَّهُ نَزَّلَهُ عَلَىٰ قَلْبِكَ
“Sema: Aliyekuwa ni adui wa Jibril, basi huyo ndiye aliyeiteremsha Qur’ani moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyezi Mungu,…” (2:97)\8
Sheikh Al-Islam Ibin Hajar 19 – Allah other Amrehemu, amesema katika kitabu cha “Fat’hu Al-Bari” Dhahiri ya mtiririko wa maneno inaonesha kuwa Mtume plwg dulo dil se ameisoma Aya ikiwa ni jibu la kauli ya Mayahudi, na wala hilo halilazimu kushuka kwake wakati huo, Amesema: Na mtazamo huo ndio tegemezi, hakika imesihi katika sababu ya kushuka kwa Aya Kisa kingine tofauti na Kisa cha Abdillahi bin Salam, ambacho amekinukuu Ahmad, At Tirmidhi na An-Nasai kutoka kwa Ibn Abbasi dic al sis, amesema;
Mayahudi walimkabili Mtume wa Allah plug que dil ole wakasema: “Ewe baba wa Kassim hakika sisi tunakuuliza vitu vitano ukitujibu vitu hivyo, hapo tutakiri kweli wewe ni Mtume kisha akataja Hadithi, na ndani yake wakauliza kilichosababisha Israili kujiharamishia mwenyewe, na alama ya Mtume al do plug qula, na kuhusu radi na sauti yake, na ni jinsi gani mwanamke hujifungua
18 Bukhari ameinukuu katika “Sahihi yake “Faslu ya Tafsiri ya Qur’an, Mlango wa: “Mtu ambaye ni adui wa Jibril.” (4120).
19 Yeye ni Ahmad bin Ali bin Muhammad Al-Kinani Al-Asqalani, Abu Al-Fadhili, Shihabuddin Ibin Hajar, ni katika maimamu wa Elimu na Historia, alijulikana sana katika fani ya Fasihi ya Kiarabu na Mashairi, kisha akageukia upande wa Hadithi za Mtume, na akasafiri Yemeni, Hijazi na maeneo mengine kwa ajili ya kusikiliza kutoka kwa Masheikh, akawa ni mashuhuri na watu wakamuendea kuchukua Elimu kutoka kwake. Na akawa katika zama zake ni nguli katika Elimu ya Kiislamu. Ametunga vitabu vingi ambavyo vimewanufaisha watu wengi. Miongoni mwa hivyo, ni: Al-Iswaba Fii Tamyizi As ‘maai As-Swahaba, Tahdhibu At Tahdhib, Lisaan Al-Mizaan, Fat’hul Al-Bari sherehe ya Swahili Al-Bukhari na vinginevyo. Alifariki mwaka (852) Hijiria. Taz. “Tabaqaat Al-Huffadh” cha Imamu As-Suyutwi (uk. 552) na “Al-A’alaam cha Azzirkali (1/178).
To read more about the Zawadi Ya Msomaji Katika Kufahamu Maneno Ya Manani book Click the download button below to get it for free
or
Report broken link
Support this Website
for websites